Sunday, November 19, 2017

MAONESHO YA KILIMO MSETO MUSOMA-MARA

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adamu Kigoma Malima, akikagua mabanda ya maonesho katika viwanja vya VI- Agro forest,Bweri Musoma.

KILIMO MSETO-MUSOMAMKUU wa Mkoa wa Mara,Adamu Malima, amesema kuwa ili kuendeleza kilimo cha mkataba cha pamba katika Mkoa wa Mara haina budi kushirikiana kwa dhati kwa vikundi vya wakulima kuwa pamoja na kuhakikisha kilimo cha pamba kinakuwa kwa kasi kwa maendeleo ya Mkoa wa Mara.

Akizungumza katika kilele cha maonesho ya kilimo mseto kwa niaba yake,yaliyomalizika jana Afisa kilimo Mkoa wa Mara, Dennis Nyakisinda alisema kuwa ili vikundi vya wakulima viweze kupata tija ya kilimo bora haina budi kituo cha sasa kilimo Mseto cha (Vi Agroforestry) cha na kanisa la AICT Dayosisi ya Mara na ukerewe kiwe kituo cha mafunzo ya kilimo mseto cha Mkoa wa Mara ambacho kitakuwa kitovu cha mafunzo ya kilimo bora na ufugaji.

‘’Kituo hiki kitakuwa kitakuwa bora cha mfano kwa masuala mbalimbali jinsi ya kupanda miti,kutambua majina ya miti, ufugaji, ukulima wa kisasa kwa ajili ya maendeleo ya mkoani hapo na nchini kwa ujumla’’Alisema Nyakisinda.


Aidha alitaka Shirika la viwanda vidogo vidogo(SIDO) Mkoa wa Mara kuhakikisha linawashaidia wajasiliamali ili wapate uwezo kwa kupata ujuzi ili waweze kuanzisha vyao wenyewe kwa ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Amesema ili kukabiliana na changamoto za tabia nchi hawana budi kuzingatia kilimo mseto ambacho ndicho kilimo pekee chenye tija.

Ameongeza kuwa wakati huu ni wakati wa mapinduzi ya viwanda na kwamba kilimo mseto ndiyo injini pekee ya maendeleo ya mapinduzi ya viwanda nchini na kwamba wakulima hawana budi kushirikiana na mashirika mbalimbali ili kuweza kufanikiwa katika kukuza uchumi wa viwanda na kuyataka madhehebu mengine kuiga mfano wa kanisa la AICT kwani bila kuwa na chakula hakuna ibada.
Amewashukuru wafadhili wa Shirika la Vi Agroforestry la nchini Sweden na Kanisa la AICT la Dayosisi ya Mara na Ukerewe kwa kuwa kipaumbele kwa kuchangia nguvu kubwa ya kupanda miti ili mkoa huo uwe na mandhari nzuri na kuzitaka na taasisi nyingine kuwaunga mkono.

Maonesho hayo ya kilimo cha mseto ya siku tatu alipambwa na mabanda ya maonesho ya bidhaa mbalimbali zikiwemo, utengenezaji wa mkaa wa udogo uliochanganywa na kinyesi cha Ng’ombe, ufugaji wa kuku wa kienyeji kwa njia ya kisasa,utengenezaji wa sabuni ya maji, mche na mbegu bora aina ya Mkombozi.


Wednesday, October 18, 2017

MWALIMU WA SEKONDARI AWA MWENYEKITI UVCCM MUSOMA VIJIJINIMwalimu wa Shule ya Sekondari ya Murangi, Martine Juma Chacha, akijieleza katika Ukumbi wa Kanisa Katoliki,kata ya Mugango, Wilaya ya Musoma Vijijini, wakati akiomba kura,aliibu mshindi kwa kupata kura 150, akifuatiwa na Jackson Nyakia kikomati ambaye alipata 124.

Saturday, June 3, 2017

Makamu wa Rais awasili Mwitongo-Butiama


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan alipokelewa na Chifu wa kabila la Wazanaki, Chifu Japheti Wanzagi, mara baada ya kuwasili alasiri katika Kijiji cha Mwitongo,alipozaliwa na kuzikwa mwasisi wa Taifa la Tanzania mzaliwa wa Mkoa wa Mara, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

EWURA yawataka wazalishaji wa Gesi kupunguza gharama za mtungi.

BUTIAMA.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imewataka wafanyabiashara wa mafuta ya gesi asilia kupunguza kiwango cha kununua gesi kwa watumiaji ili wananchi wa kipato cha chini waweze kuhimiri bei ya gesi na kuwasaidia katika kupunguza matumizi ya ukataji miti ovyo unosasabisha kutoweka kwa uoto wa asili ambapo kwa sasa watumiaji wa mkaa wanaongezeka na kusababisha mazingira kuharibika.


Akizungumza na waandishi wa habari katika banda la Mamlaka hiyo, kuwanja wa Mwenge-Mwitongo Wilaya ya Butiama, Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) Kanda ya Ziwa,Nyirabu Musira,amesema kuwa upunguzaji wa bei utasababisha upungufu wa matumizi ya mkaa ambao ulikuwa ukitumiwa na wananchi.

Hii ni katika maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa inafanyika kijijini Mwitongo Wilaya ya Butiama alipolelewa na kuzikwa hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Leo kuna kongamano la hifadhi ya Mazingira linaloendelea katika Ukumbi wa Romani Katoliki jirani na kanisa alilokuwa anasali Baba wa Taifa, ambapo Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba.